Tuesday, 25 June 2013

JE, NI SUMU AO LA?

JE, NI SUMU AO LA?

Watu wengi wanaowaona waganga wa asili wanawajulisha kwamba walitumia sumu ila hawajuwi mahali ambapo waliweza kutana na watu walio wapa hio sumu. Hatunabudi kujuwa kwamba kuna magonjwa kadhaa ambayo zina alama nyingi zinazofanana. Magonjwa mengi yanagunduliwa kiisha tuu kufanya examen ya laboratoire. Ndiyo maana hatupaswi kukimbilia tuu kusema kwamba tulikula sumu bila kujihakikishia kupitia majibu ya examens za laboratoire.

Watu wanao uguwa magonjwa yafuatayo, wanaweza kudanganywa  kwamba walekula sumu na wengi, mara nyingi, wameambiwa kwamba ni majirani wasiowapenda ndio chanzo cha sumu hizo:
  • Vidonda kwenyi estomac-ulcères- ama ugonjwa wa estomac tuu,
  • Homa ya matumbo ama fièvre typhoide.
  • Ugonjwa wa mkoyo ambao unaitwa infections urinaires.
  • Matatizo inayotokana na chakula ama complications alimentaires.
  • Shida ya chakula isiyopatana na blood group ama groupe sanguin ya mtu.
  • Kuhara na kutapika.
  • na mengine kadha wa kadha.
Tujulishe ya kwamba hata watu wanaouguwa magonjwa yasiyopona kama vile sida, wanadanganywa saana na "madaktari bandia" kwamba walitumia sumu na kwa hiyo ingelikuwa muhimu kwao wangeanza kutibiwa nao kupitia majani ya asili.

Tujuwe ya kwamba mtu anapotumia dawa ya sumu ijapokuwa hana hiyo sumu mwilini, hapo ndipo tunaweza sema kama alikula sumu sababu ametumia dawa ya ugojwa asiyokuwa nayo. Hapo sasa anaji intoxiquer na kuna hatari nyingi kutokana na hali hii sababu hajuwi lile analolifanya na mganga wake naye hamsaidii hata kidogo anapompa dawa bila kujihakikishia kimbele mtu huyo anauguwa nini.

Asante saana.

Jean-Jacques Shamsaf