Thursday, 14 July 2011

KWA NINI SI VIZURI KUTUMIA DAWA ZA ASILI KABLA YA KUONA MGANGA?

Dawa za asili ni nzuri sana kwa kutiba magonjwa mengi. Tangu myaka mingi iliyopita katika historia ya wanaadamu, matumizi ya dawa za asili ilikuwa njia mojawapo iliyowasaidia wagonjwa kadhaa. Hata kwa wakati wetu,  dawa tunazoita za kizungu zinapoonekana hazitendi, wagonjwa wengi wanapata matibabu wakitumia majani ama dawa za asili.

Lakini tungejibu kwenyi swali hii: je dawa za asili ni nzuri kwa matibabu? Ni kweli jibu inaweza kuwa ndio lakini tunapaswa kujuwa kwamba kwa njia moja ao jingine dawa za asili zisipotumiwa kwa njia inayo sawazika, zinaweza kuwa sumu kwetu. Kwa hiyo, tutafaya vema ikiwa tutajikaza kutumiya dawa kiisha kuwaona waganga ama madaktari (wanaojulikana kiserkali) kwa sababu kuna alama za magonjwa zinazofanana. Kwa mfano, inajulikana, na hata kisayansi,  kwamba mtu anaweza fikiria amekuwa na tumia dawa za kutunza mafuwa anapotowa makamasi. Lakini tusisahau kwamba kuna magonjwa megine kama vile magonjwa fulani ya maini(liver katika lugha ya kiingereza) inaweza kuwa chanzo cha kutoa makamasi. Pia, kuna wale ambao wanaouguwa ugonjwa unaoitwa gastrite(kifaransa ama gastritis kwa lugha ya kiingereza). Wengi kati yao wanafikiria kwamba walipewa sumu. Kwa hiyo, wamoja wanatumiya madawa za kutapikisha sumu bila kupimwa wakifikiria kwamba watajiepusha na matokeo mabaya ya sumu. Lakini, kwa mshangao, wanaendelea kuuguwa kwa sababu wapowana jiwekya akiba ya madawa yasiyo faa mwilini kiisha yanawaletea shida. Ndiyo maana tunahitaji uangalifu mbele ya yote.

Watu wengi wanajikuta wamekuwa wagonjwa saana kwa sababu yakutumiya dawa za asili kwa njia isiyofaa.

Na waganga wengi wamewapa wagonjwa madawa za asili bila kufikiria chemical properties zinazoweza kuwa ndani yazo,  shauri za kiganga, kwa vyovyote bila uangalifu.

Tukifikiria mambo ambayo tunatoka  kuzungumzia, tutafanya matibabu kupitia dawa za asili kuwa moja wapo ya njia nzuri kwakutunza afya yetu na ya jamii.

1 comment:

  1. kwa sa babu dawa za asili zina tumiwa bada yaku pimwa kwa lab, dosage zayo hazieleweki vizuri. na wanazo zipana siwaganga walio soma maranyingi hawana elimu ya dawa wanazo pana. Ya jean merci kwa blogg ya mashi

    ReplyDelete